Serikali mkoani Kilimanjaro inaelekea kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 20 baina ya uongozi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA na wananchi wa maeneo yanayozunguka uwanja huo baada ya Serikali kusema kuwa itafanya tathmini, kuwalipa na kuwaondoa wananchi waliovamia eneo la uwanja huo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Kia, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu anaeleza kuwa “eneo hili lina hati ya miaka 99 kwa ajili ya kuendeleza kiwanja cha ndege cha KIA ambacho manufaa yake yatakuwa miongoni mwenu”.
“Tutakuja kufanya tathmini kwa kupima eneo lote la uwanja wa ndege KIA halafu tujue nani yuko ndani ya uwanja, nani yuko nje ya uwanja, yule ambaye yuko ndani ya uwanja huyo ndiyo tutadili naye, ambaye yuko nje ya uwanja hatutakuwa na shughuli naye” ameongeza RC Babu
Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi wa kata ya Kia kutoa ushirikiano kwa Serikali wakati wa kufanya tathmini hiyo itakayo fanyika Novemba 09, 2022 kuwabaini wananchi waliopo ndani ya eneo la uwanja huo ili walipwe fidia kupisha eneo hilo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi amewataka wananchi hao kuhakikisha kuwa wanatengeneza mustakabali wa maelewano kwa kudumisha amani katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kukubaliana na uamuzi wa Serikali ambao una manufaa kwa pande zote mbili.
“ninyi watu wa Kia, leo tunakusudia mtengeneze amani ndani ya Kia, kwamba tunatakiwa tulete amani hapa na wenye kuleta Amani hapa wa kwanza ni nyie, msipotengeneza Amani hapa hamuwezi kuipata mahali pengine, na tukifikiria kuipata mahali pengine sio kwa njia ambayo ni sahihi”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai