Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya amefanikiwa kurejesha kwa wananchi wa vijiji vinne Shamba la Fofo lenye ukubwa wa ekari 46.6, lililopo katika kijiji cha Narumu kata ya Machame Narumu lililokuwa na mgogoro kati ya Piter Karanti na wanakijiji hao.
Sabaya amechukua hatua hiyo leo katika mkutano na wananchi wa kijiji hicho uliofanyika kijijini hapo baada ya kuwepo kwa mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya wananchi hao na bwana Piter Karanti pamoja na wenzake 48 ambao walijimilikisha shamba hilo kinyume na taratibu.
Amefikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza pande zote mbili na kujiridhisha huku akisema kuwa kw mujibu wa hati ya msajili shamba hilo ni mali ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania hivyo hawana haki juu ya umiliki na amewataka wananchi hao 48 waliokuwa wamejimilikisha shamba hilo kuhakikisha ndani ya siku saba wanaboma nyumba walizozijenga ndani ya shamba hilo na kwamba kuanzia sasa ni mali ya wananchi wa vijiji hivyo.
Amesema "Kwa mujibu wa ofa, hati ya msajili ni mali ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, lile shamba serikali imefanya majaribio maalumu ya kuwakabidhi vijiji hivi vinne,orori usari,Tela na mlama, lakini kwa mara zote kikundi hiki, kimejitahidi ukimbia mahakamani ili kuwazuia wananchi hawa kupata haki zao, kama mtu amejenga nyumba yakudumu maana yake huyo amejitaftia matatizo mwenyewe".
" Kwa maana hiyo Piter na wenzake kwa miaka hiyo yote wamekuwa wakipora haki ya wananchi, Mh. Rais amekuwa akielekeza kwamba hii ni mali ya wananchi wote, kikundi cha watu wachache kisichukue na kujimilikilisha mali ya watu wote, sasa leo natangaza ni mali ya wananchi wa vijiji hivi, Jambo la pili ninaelekeza kama kuna ujenzi wowote umeendelezwa pale shambani nemdeni kabomoeni nyumba zenu wenyewe ndani ya siku saba, kumbe kuna ushahidi wamejipatia shamba hili kwa idanganyifu" Amesma Sabaya.
Aidha amemwagiza Mkuu wa polisi wilayani Hai kuwashikilia Mwenyekiti wa kijiji na wenzake watatu ambao wamekuwa wakihusika na jambo hilo huku akimtaka mwanasheria wa serikali wilayani hapo kuwaandikia barua uongozi wa bank ya CRDB kutaka kujua utaratibu uliotumika kuwamilikisha watu hao shamba hilo.
Imeelezwa kuwa chanzo cha mgogoro huo ambao ulianza mwaka 1977 ni kuibuka kundi la Bw.Piter na wenzake 48 kukabidhiwa shamba hilo na Bank ya CRDB baada ya kulipa deni la zaidi Tsh.laki moja lililokuwa likidaiwa na bank hiyo kwa Dr. Anthony Phones ambae alikuwa akimiliki shamba hilo licha yachama cha ushirika Narumu Manushi kushinda tenda iliyotangazwa na bank ya CRDB,lakini wakashindwa kulipa deni hilo hali iliyoilazimi bank hiyo kuwakabidhi shamba hilo Piter na wenzake 48.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai