Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa skimu za umwagiliaji kwa lengo la kuimarisha kilimo nchini.
Mhe. Rais Samia ametoa kauli hiyo baada ya mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafue kumuomba kutenga fedha kwaajili ya kusaidia ukarabati wa skimu za umwagiliaji zilizoharibiwa na mafuriko na kusababisha wakulima katika baadhi ya maeneo wilayani humo kushindwa kuendelea na Kilimo cha Umwagiliaji.
“tayari waziri wa fedha amekwisha kwenda kutafuta fedha za umwagiliaji na skimu uliyoizungumzia mbunge itakuwa miongoni mwa skimu hizo”.amesema Rais Samia.
Pia Mbunge Saashisha alimshukuru Mhe Rais juu ya ahadi yake ya ujenzi wa soko la kwasadala ambalo pamoja na mambo mengine kitakuwa na kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao.
"Mhe. Rais ulituahidi soko la Kwasadala tayari tumekwisha tengeneza ramani ambayo ndani yake kutakuwa na viwanda vya kuongeza thamani mazao na vya kufungasha, nikuombe sana leo ukitamka neno wataanza kulijenga lile soko na akina mama wanatamani kufanya biashara katika soko la kisasa kabisa".
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai