KERO ya ukosefu wa vifaa vya kujifungulia kwa kinamama wajawazito katika zahanati ya Kyeri kata ya Machame Magharibi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imetatuliwa na serikali baada ya kupatiwa vitanda 12 vya kupumzikia pamoja na vitanda vya kujifungulia.
Vitanda hivyo pamoja na vifaa vya kujifungulia kwa wanawake wajawazito vimetolewa na Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini vyenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa ni mchango wa faida wanazopata kutoka wateja wao.
Akipokea vitanda hivyo , Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema kuwa upatikanaji wa vitanda hivyo kutoka kwa wadau hao unatokana na ombi lililotolewa na wananchi wa kijiji hicho kwa mkuu mnamo Novemba 26 mwaka huu.
Ole Sabaya amesema serikali ya Awamu ya Tano iko kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuondokana na huduma duni za kujifungua kwa kinamama wajawazito.
Akikabidhi vitanda hivyo Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro, amesema huo ni utaratibu wa kutenga asilimia kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya na elimu kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma nzuri za afya na elimu.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Hai, Dkt. Irine Haule ameishukuru benki hiyo pamoja na serikali kwa kuona sehemu ya afya inahitaji msaada wa vifaa na kuwahakikishia kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kupunguza vifo vya watoto wadogo na wakina mama wanapojifungua.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai