Zaidi ya wananchi 350 ambao hufika kupata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Hai kila siku wanatarajia kunufaika na huduma bora za kiafya zitolewazo hospitalini hapo baada ya serikali kuendelea kuboresha huduma hizo ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba mbalimbali.
Mapema hii leo mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amekabidhi mashine ya X - Ray yenye thamani ya shilingi milioni 196 ambayo itatumika katika kutolea huduma za mionzi hospitalini hapo.
Akikabidhi mashine hiyo mbunge Saashisha amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo ameendelea kutoa fedha za miradi mbalimbali katika wilaya ya Hai ambapo imepelekea wananchi wa wilaya ya Hai kuondokana na adha mbalimbali walizokuwa wakikumbana nazo hapo awali.
"Leo hii tuna X -ray Mashine mpya, ICU yenye vifaa vyote vya kisasa, maabara pamoja na wataalam wa kutosha, hakika hii ni dhamira nzuri ya rais Dkt. Samia katika kutuhudumia wananchi wa Hai". Alisema Saashisha Mafuwe.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga amesema kuwa watahakikisha kuwa wanatunza vifaa hivyo pamoja na miundombinu yote inayotolewa na serikali ili kuhakikisha kuwa wilaya na wananchi wananufaika kutokana na huduma bora.
Akizungumza kwa niaba ya chama cha mapinduzi CCM katibu wa itikadi na uenezi Ndg. Muddy Msalu amesema kuwa maboresho yanayoendelea ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 na kuwaomba wananchi kuzidi kukiamini chama cha Mapinduzi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai