Serikali imetoa zaidi ya shilingi million 48 Kwa ajili ya ujenzi wa choo Bora katika shule ya msingi Bomang'ombe iliyopo katika Kijiji cha mkombozi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro
Akizungumza wakati wa zoezi la kukagua eneo la ujenzi wa Choo hicho na kutambulisha Mradi,Diwani wa kata ya masama kusini Mh Cedrick Pangani ameshukuru jitiada na ushirikiano uliopo kati ya viongozi na wananchi wa eneo hilo.
Kwa upande wake Emaculata Mgaza mratibu wa mradi wa usafi na usambazaji wa maji vijijini amesema fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa choo bora ambacho pia kitajumuisha na ujenzi wa chumba maalum cha watoto wa kike cha kujistiria chenye vifaa ndani Kama vile taulo za kike,eneo la kuchomea taka lakini pia chumba kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum
Sambamba na hayo choo hicho chenye matundu ya vyoo takribani 15 kitajengwa ikienda sambamba na ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji.
Hata hivyo kaimu Afisa Elimu msingi Jafari Zaidi ametoa Kwa wananchi kuutoa taarifa wanapoona changamoto yoyote katika mchakato huo katika ofisi ya mawasiliano,ofisi ya mipango na zingine ili kufanikisha mradi huo..
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai