Wamiliki wa shule za msingi za binafsi wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kinga tiba linalotarajiwa kufanyika tarehe 19/03/2020, na kwamba zoezi hilo linaoendeshwa na serikali limelenga kuimarisha afya za watoto nchini.
Akizungumza wakati wa kikao cha mpango mkakati wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella amemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisa kuwa shule hizo zinashiriki zoezi hilo ili watoto wa wilaya ya Hai wapate kinga tiba na chanjo kwa asilimia 100.
Wella ametoa agizo hilo baada ya taarifa ya utekelezaji wa mpango huo mwaka jana kuonesha kuwa baadhi ya wamiliki wa shule za msingi binafsi walitoa maagizo kwa wasimamizi wa shule kutoruhusu watoto kupewa dawa za minyoo na kichocho.
Awali akiwasilisha taaifa hiyo mratibu wa mpango wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Apolnary Tesha amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwazuia watoto wao kushiriki katika mazoezi kama hayo kutokana na uvumi juu usalama wa dawa hizo na kuwahakikishia kuwa kabla ya zoezi lolote kufanyika Wizara ya Afya inafanya kwanza utafiti juu ya usalama wa afya za watumiaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai