Wananchi wa kijiji cha Mbosho kata ya Masama Kati wilaya ya Hai wamepokea fedha za mradi wa BOOST shilingi 101,082,832.00 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi mafeto.
Akizungumza Katika kikao hicho cha utambulisho wa mradi huo Jafari Zaidi ambae ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Elimu Ms na Awali Wilaya ya Hai amewataka wananchi hao kuulinda mradi huo dhidi ya wizi wa vifaa vya ujenzi.
Naye Mkuu wa Idara ya Mendeleo ya Jamii wilaya ya Hai Robert Mwanga amewataka vijana wa eneo hilo kutumia fursa ya Ujenzi huo kufanya kazi ili kujiongezea kipato.
Nae Mtendaji wa kijiji hicho Happy Piter Titto ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Mh Rais Samia Suluhu Hasan kwa kuwapelekea fedha hizo za mradi wa BOOST ambazo zitasaidia maboresho makubwa katika shule yao ya msingi Mafeto.
Nae Mwananchi wa ķijiji hicho Agness Salimu Kweka ameishukuru Serikali na kuomba ukarabati na ujenzi huo uendelee katika shule zingine.
Akijibu hilo Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi na Awali Jafari Zaidi amesema Serikali kwa mwezi Julai 2025 pekee imetoa 1,553,665,664.00 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule za Msingi wilayani Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai