Serikali katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kwa Tito ndani ya siku 14 ili kusogeza huduma za afya kwa wananchi wa Kijiji hicho.
Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya akiwa kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya afya katika wilaya hiyo.
Sabaya amewalaumu wataalamu kwa kuchelewa kufanya maamuzi sahihi katika kukamilisha ujenzi huo kwani fedha za kazi husika zimeshaletwa kwa ajili ya kazi hiyo.
“Rais Magufuli ameleta fedha ili ziwasaidie hawa wananchi wanyonge kwa kuwaboresea huduma za afya; mfanye mnavyoweza hili jingo liwe limekwisha ndani ya siku 14” Amesema Sabaya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Weruweru Swalehe Msengesi amepongeza maamuzi ya Mkuu wa Wilaya huku akiongeza kuwa wananchi wamechangia zaidi ya shilingi milioni nne ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ujenzi wa zahanati hiyo.
Naye Mtendaji wa Kijiji cha Kwa Tito Olivia Musamba amesema kukamilika kwa zahanati hiyo kutasaidia kutoa huduma za afya kwa zaidi ya wakazi 1000 wa kijiji hicho na wengine kutoka vijiji jirani ambao kwa sasa wanapata huduma kwenye zahanati za kijiji jirani au hospitali ya wilaya huku wakikabiliana na changamoto ya umbali.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai