Serikali Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imedhamiria kuanzisha soko la madini katika eneo la uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ili kuwa sehemu ya uhakika ya kuuzia madini ya aina mbalimbali kwa bei elezekezi.
Akikagua eneo hilo Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema soko hilo la kisasa ,litakuwa na aina zote za
madini yanayopatikana Tanzania na pia litawasaidia wachimbaji wadogo kutambua bei elekezi ya serikali ya ununuzi
wa madini hatua ambayo itawasaidia kunufaika nayo.
“Soko hili kwa sasa tutalianzisha ndani ya uwanja huu wa ndege wa KIA na tunatarajia ndani ya siku saba soko hili
litakuwa limekamilika kwa kuanza kutoa huduma kwa wachimbaji ”amesema Mkuu wa Wilaya.
Ole Sabaya amesema kuwa, soko hilo litarahisisha huduma za uuzaji na ununuzi wa madini ambapo huduma zote
zitatolewa ndani ya jengo moja hivyo kuokoa muda wa wauzaji na wanunuzi wa madini
“Tukijenga soko hili hapa advantage yake(faida ) ni kwamba mtu yoyote akifika hapa anaelezwa umeingia
Tanzania na kwamba madini yote yanapatikana hapa, madini ya tanzanite yanapatikana Mirerani unayakuta
hapa,madini ya almasi kutoka mwadui yanapatikana hapa ”amesisitiza Sabaya
Kwa upande wake, afisa madini mkazi mkoa wa Kilimanjaro, Fatuma Nkyando amesema soko hilo litasaidia%
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai