Mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Amir Mkalipa ameipa ameipongeza Taasisi ya Tanzania Islamic Teaching Association (TISTA) Wilayani hapo kwa kuwasaidia watoto katika swala zima la maadili na malezi ili waje kuwa raia wema wa Watanzania
Mkalipa ametoa pongezi hizo wakati wa semina ya usimamizi wa mtihani wa Taifa wa EDK wa Darasa la saba iliyofanyika katika ukumbi wa Misikiti wa Safii Bomang'ombe Wilayani humo, na kuhudhuria na Walimu wa shule ya Msingi , Sekondari na Walimu wa Madrasa
Mkalipa amewataka Walimu hao kuendelee kufundisha kujitoa kwa hali na mali kufundisha watoto na kuwaandaa na kusome elimu ya Dini yao lakini na kufanye juhudi kubwa kusoma masomo mengine ili waweze kufaulu
Amesema lengo lao ni zuri Kwa sababu wanataka kuweka nguvu katika kuhakikisha watoto wanafanya vizuri masomo ya Dini na masomo mengine yote kuhakikisha watoto wanafaulu katika Wilaya hii
"Ni kweli niwaongeze taasisi hii na malengo yake ni mazuri ,niwatie moyo na kuwaunga mkono ,kwa sababu pia wanakusanya michango kwa ajili ya kuwasaidia kufanikisha watoto wasiojiweza kusoma shule mbali mbali ili ni jambo kubwa na la kupigiwa mfano na sisi tujitoa kama Serikali "amesema Mkalipa
“Wito wangu ni kuhakikisha mambo yote yanakwenda vizuri na kila mwenye uwezo wa kuchangia sehemu ili watoto wa kitanzania waweze kupiga hatua “
Kwa upande wake sheikh wa Wilaya Masuud Mbowe, amesema vipindi vya Dini Shuleni vinasaidia kuwajenga watoto kukua katika maadili mazuri.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai