Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilaya ya Hai imeanza zoezi la kusikiliza kero za wananchi kupitia mpango wa programu ya TAKUKURU RAFIKI ambapo wameanza na kata ya Masama Rundugai wilayani humo.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Masama Rundugai wakati akipokea kero za wananchi hao, Afisa wa dawati la Elimu kwa umma TAKUKURU wilaya ya Hai Dayness Muro amewataka wananchi wa wilaya hiyo kutoa ushirikiano kwa kufichua vitendo vya rushwa.
"Wananchi wanapoibua zile kero tunakaa tunaona ni namna gani ya kuweza kuzitatua, kwahiyo kupitia programu ya TAKUKURU RAFIKI tunaona katika kusikiliza kero na kuwa karibu na wananchi kusikiliza changamoto zao tunaweza kufikia malengo ya Mhe. Rais kwa maana ya kuwa na utawala bora"
Wananchi waliofika kwenye mkutano huo wamezilalamikia bodi za maji wilayani humo kwa kuwabambikizia bili kubwa za maji ambapo wameiomba TAKUKURU wilayani Hai kuchunguza sakata hilo.
Kwa upande wake Afisa wa TAKUKURU wilayani humo Salome Sway ameeleza kuwa kero zinazotolewa na wananchi zitatafutiwa ufumbuzi wa haraka ili kuepuka kutengenezwa kwa viashiria vya rushwa.
Hata hivyo Disemba, 2022 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Jenista Mhagama alizindua rasmi program ya TAKUKURU RAFIKI ambayo itatoa fursa kwa kila mtanzania kushirikiana na Serikali kupitia Takukuru kutekeleza jukumu la kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo ni kikwazo kikubwa cha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai