Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilaya ya Hai imewataka Wagombea na Wananchi wilayani humo kujiepusha na vitendo vya rushwa hasa kuelekea katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika Kipindi cha Siku Mpyaa kinachorushwa na Radio Boma Hai Fm Afisa takukuru wilaya ya Hai Julius Msoka amesema katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ni vyema wagombea wakazingatia maelekezo yanayotolewa kupitii sheria za uchaguzi.
Aidha Msoka amewataka wapiga kura na wananchi kutoa taarifa za matukio yanayoashiria vitendo vya rushwa lengo likiwa ni kupata viongozi waadilifu watakaochaguliwa na wananchi bila kuwepo aina yoyote ya ushawishi.
“Takukuru imekuwa ikipokea na kufanyia kazi taarifa nyingi zinazoletwa na wananchi na mara zote wale wanaotupa taarifa hatuwezi kuwataja”. Amesisitiza Msoka.
Naye Salome Swai ambaye pia ni Afisa TAKUKURU katika Wilaya ya Hai amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya serikali ikiwemo TAKUKURU kufichua makossa yanayohusu rushwa yanayotendeka kwenye jamii huku akiwakumbusha wananchi kuwa wao ndiyo waathirika wakuu.
Kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono Swai amesema kuwa vitendo vinavyohusiana na aina hiyo ya rushwa mara nyingi hufanyika kwa namna ya usiri hivyo kuwataka waathirika kuvunja ukimya na kujitokeza kutoa taarifa kwenye mamlaka ili wahusika wachukuliwe hatua stahiki.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai