MENEJA wa TaNesco, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Mhandisi Daniel Kyando amesema Serikali imeweka mkakati wa kuvifikia vijiji vyote ambavyo havijapata huduma ya umeme kama ambavyo iliahidi.
Kyando ameyasema hayo wakati akijibu swali la diwani wa kata ya Weruweru Abdalla Chiwili aliyetaka kujua ni lini shirika hilo litakamilisha zoezi la kuwaunganishia umeme wananchi ambao hawajafikiwa na huduma hiyo.
Akitoa ufafanunuzi wa namna ya kukamilisha huduma hiyo katika kikao cha baraza la madiwani Mhandisi Kyando amesema serikali imeweka mikakati madhubuti katika mwaka wa fedha ujao kuhakikisha kuwa inakamilisha zoezi hilo kwa vijiji vyote ambavyo bado havijapata umeme wilayani humo.
Amesema katika wilaya ya Hai , vitongoji 40 kati ya 262 ndivyo havijafikiwa na huduma hiyo ambapo tayari serikali imetenga fedha katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kumalizia vitongoji hivyo .
Ameeleza kuwa, wananchi ambao walikuwa wamelipia fedha 27000 kabla ya mabadiliko ya bei ya kuunganishwa hawatalipia tena wala kuongeza fedha na badala yake wataendelea kusubiri kupata huduma hiyo pindi zoezi hilo litakapoanza.
Hata hivyo amefafanua kuwa wakazi wa kata za mamlaka ya mji mdogo ambazo ni kata ya Muungano, Bondeni na Bomang’ombe ndio watakaolazimika kulipa kiasi cha shilingi laki tatu huku kata zingine zitaendelea kulipia kiasi cha shilingi elfu ishirini na saba tu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai