Kaya 4,478 wilayani Hai zimenufaika na mahindi ya bei nafuu yaliyotolewa na Serikali kupitia wakala wa Taifa wa chakula NRFA kwa lengo la kusaidia wananchi kupunguza ukali wa maisha kufuatia kupanda kwa bei ya mahindi sokoni kutokana na kukosekana kwa mvua kwa misimu miwili mfululizo.
Afisa maafa wilaya ya Hai Msafiri Msuya ameeleza kuwa hadi sasa wilaya hiyo imeshapokea tani 420 za mahindi na kuzigawa kwa wananchi kupitia viongozi wa vijiji na vitongoji kwa bei ya shilingi 44,000 kwa mfuko wa kilo 50.
“Niwaombe wananchi watumie fursa hii kwa ajili ya kujipatia hayo mahindi na wayatumie vizuri kwa matumizi ya nyumbani hapa tulipo hatujui kwamba msimu unaokuja, je tutalima? tutavuna? Kwa hiyo bado niwasihi, mahindi haya wayanunue na wayatunze”
“kwa upande wa viongozi hasa hawa wa vijiji nitumie fursa hii kuwaomba wawe waaminifu kwamba mahindi haya yamekuja yanauzwa kwa bei nafuu ukilinganisha na bei ya sokoni, basi zile orodha ambazo wanaziandaa kule vijijini, wao ndio wako na jamii watusaidie kutuletea orodha sahihi ya wahitaji kweli kweli na wasifanye upendeleo”
“kama mtu hawezi kununua mfuko wa kilo 50 bado kule katika ngazi ya kitongoji wanaweza wakaungana familia kadhaa wakaorodheshwa wakajichanga na kila mtu akaweka kumbukumbu yake baadaye zikijumlishwa zinaweza zikafika mifuko miwili au mitatu wakagawana”
Ikumbukwe kuwa mahindi hayo ya bei nafuu ambayo ni mkombozi wa wananchi hususani wa wilaya ya Hai huuzwa kwa 44,000 kwa mfuko wa kilo 50 na 88000 kwa mfuko wa kilo 100, huku bei ya sokoni huuzwa kwa shilingi 150,000.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai