Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 162 kwa vijiji 70 ambavyo vitatumika kama vitendea kazi kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ajira ya muda kama vile barabara za jamii, upandaji miti ,mifereji ya umwagiliaji ,pamoja na bwawa.
Hayo yalisemwa Machi 06,2023 na Mratibu wa kunusuru Kaya maskini (TASAF) Halmashauri ya Hai Michael Momburi wakati wa zoezi la utoaji wa vifaa hivyo ambavyo ni Sururu, majembe, reki pamoja na chepe.
Momburi alisema katika kipindi hiki wanatekeleza miradi ya kutoa ajira ya muda kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini ajira hizo zinalenga Kaya ambao umri wao unaanzia umri wa miaka 18 hadi 65 na wana uwezo wa kufanya kazi wa sio na matatizo ya kiafya na katika kutekeleza hilo wana miradi 70 katika vijiji 62 na mitaa 17 ya Kata 17 za wilaya ya Hai .
Utekelezaji huo umeanza Februari 27,2023 na utatekelezeka kwa siku 60 hivyo wanategemea hadi Juni 26,2023 miradi yote itakuwa imekamilika, na mara baada ya miradi hiyo kukamilika vifaa hivyo ni mali ya kijiji husika kukamilika kwa miradi hiyo sio tu itawanufaisha wanufaika wa TASAF bali ni jamii nzima.
Nao baadhi ya wanufaika wa mpango huo akiwemo Oliva Lyimo na Liliani Mushi wameishukuru Serikali kwa kutoa ajira hizo za muda kwani wameweza kunufaika kwa kulipa ada za watoto, kukodi shamba kwa ajili ya kulima , na kununua mifugo biashara.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai