Chama cha mapinduzi wilaya ya Hai kimefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa madarasa pamoja na nidhamu ya matumizi ya fedha katika shule ya msingi Sanya station iliyopo kata ya Kia wilayani humo.
Shule hiyo imejenga vyumba viwili vya madarasa pamoja na kutengeneza madawati 46 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 40.
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya chama hicho mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai Wang'uba Maganda amesema amefurahishwa na namna uongozi wa shule hiyo ulivyoonyesha uaminifu na uadilifu kwenye matumizi ya fedha za Serikali katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
"Niwapongeze sana watu wa Sanya station kwa uaminifu na nidhamu mliyoonesha kwenye matumizi ya fedha za Serikali katika ujenzi wa vyumba hivi vya madarasa, mkurugenzi naomba ikija tena hela nyingine muikumbuke tena shule hii ya sanya station katika ufalme wenu, peleka fedha kwa mtu mwaminifu"
Naye katibu wa CCM wilaya ya Hai Kumotola Kumotola ameeleza kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo unapofanyika kwa uaminifu inasaidia kuokoa fedha za Serikali ambazo zinaweza kusaidia utekelezji wa miradi mingi zaidi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai