Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai ndugu Yohana Sintoo amewaagiza wakuu wa idara kutumia vema mafunzo waliyoyapata ili kuboresha utendaji wa kazi za kila siku na kuzuia viashiria hatarishi na ubadhilifu wowote unaoweza kujitokeza kwenye halmashauri.
Mkurugenzi ametoa agizo hilo wakati wa mafunzo ya usimamizi wa viatarishi na viashiria vya ubadhilifu katika mamalaka ya serikali za mitaa yaliyotolewa na timu ya wataalam kutoka sekretarieti ya mkoa wa Kilimanjaro.
Sintoo pia ameushukuru uongozi wa mkoa kwa kutoa mafunzo hayo hasa katika kipindi hiki ambacho taasisi na jamii inakumbwa na changamoto mbalimbali na kwamba mafunzo hayo yatasaidia katika kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya changamoto kabla ya kuleta madhara.
Akitoa mada katika mafunzo hayo ndugu Julius Msoka amewataka watumishi wa umma kufuata sheria,kanuni,taratibu na miongozo mbali mbali katika kutekeleza majukumu yao hasa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuiwezesha serikali kukamilisha miradi kwa wakati inayoendana na thamani na kuepuka makosa yanayoweza kuwasababisha kuchukuliwa hatuwa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai