Jamii imetakiwa kushirikiana na serikali ili kutunza vivutio mbali mbali vilivyopo kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti kwa lengo la kuhifadhi mazingira.
Rai hiyo imetolewa na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai David Lekei wakati wa ziara ya timu ya wataalam wa wilaya hiyo kutembelea na kukagua maeneo mbali mbali yenye vivutio kwa lengo la kuweka mikakati ya kuboresha maeneo hayo.
Amesema endapo maeneo hayo yatatunzwa vivuri yatakuwa chanzo cha ajira kwa vijana wengi wa wilaya ya hai.
“Baada ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuiweka Tanzania hewani watanzania tumepata fursa ya kupata watalii tena hasa hapa kwetu Kilimanjaro tena wilaya ya Hai hapa ndo kitovu cha utalii maana ndege zote zinazokuja kwa ajili ya utalii lazima zipitie hapa kupitia uwanja wa ndwge wa Kilimanjaro (KIA) ambao upo ndani ya wilaya yetu tena wanapita huku huku sasa na hapa lazima tupatengeneze waje na hapa”amesema Lekei.
Kwa uapnde wake Afisa Utalii Amani Temu amesema kwa sasa wanafuatilia historia kamili ya eneo hilo ili watalii watakapo anza kutembelea eneo hilo wapate na historia iliyojitosheleza.
Daraja hilo la mjerumani ni rasilimali amabyo ipo eneo la kijiji cha kwasadala ambalo limejengwa mwaka 1906 hadi 1912 lipo kwa ndani kidogo pembeni ya daraja la mto kikafu lilijengwa na mjerumani miaka mingi iliyopita na linatumika mpaka hivi sana.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai