Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe.Lazaro Twange amewaagiza wakandarasi wote wanaotekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara wilayani Hai kufanya kazi na kukamilisha miradi hiyo kwa muda uliopangwa.
Amesema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya Barabara zinaendelea na utekelezaji katika wilaya ya Hai ambapo amepongeza Kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuridhika na utekelezaji wa Miradi hiyo yenye thamani ya zaidi Bilioni 8. Ameongeza kwa kuwataka Wananchi wote kuona kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan.
Nae Manager wa TARURA Wilaya ya Hai Fuya Francis ameeleza Kasi ya miradi hiyo inavyoenda kwa nguvu kubwa inayotoka serikali kuu, vile vile ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti katika ujenzi wa miundombinu ya Barabara.
Ameongeza kwa kutoa wito kwa Wananchi wote wa Wilaya ya Hai kutunza na kulinda miundombinu mbalimbali inayotekelezwa kwa kufuata kanuni na maelekezo yote yanayotolewa na TARURA ili kuendelea kuleta maendeleo kwenye Miundombinu ya Barabara katika Wilaya ya Hai kwa juhudi kubwa za Fedha za serikali.
TARURA Wilaya ya Hai imeendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara za Mijini na vijijini ambazo zinajengwa kwa awamu ambazo ni Barabara ya (Bomang'ombe - TPC - Kikavu Chini), kwa kilometer 3.5 Kwa kiwango cha lami kwa awamu ya kwanza, Barabara ya (Makoa- Takri- Mferejini) km 18.3 Kwa kiwango cha Lami na Taa, Barabara ya Kwasadala-Tema-Mwalukeni-Ng'uni-Isuki-Lukani-Jiweni Mashua Km 35.06 Kwa kiwango cha changarawe,yenye thamani ya Bill.8.5.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai