Wananchi kijiji cha Ng’uni kata ya Masama kati wilayani Hai wamepatiwa mafunzo ya ufugaji wa nyuki wadogo pamoja na aina zake mafunzo ambayo yamefanyika katika ofisi ya kijiji hicho lengo ikiwa ni kupata ujuzi na mafunzo ya aina mbali mbali yanayohusiana na nyuki.
Akiongoza mafunzo hayo kijijini hapo Afisa Nyuki wilaya ya Hai Joyce Kombe amesema kuwa lengo kubwa la serikali katika kutoa mafunzo hayo ni kuweza kuwaunganisha wanavikundi na wafugaji nyuki katika masoko mbali mbali.
Ameongeza kuwa ufugaji wa nyuki una faida mbili ikiwemo kutunza mazingira pamoja na kuongeza pato la kaya huku akiwahimiza wananchi kuchangamkia fursa ya kufuga nyuki ili waone manufaa yake hasa pale watakapobadilisha hali ya uchumi wao.
Naye makamu mwenyekiti wa chama cha wafuga nyuki wilayani Hai Eduard Meena amesema kuwa dhumuni ni kuhakikisha kuwa asali inapatikana kwa wingi kwa kutumia njia bora ya ufugaji wa nyuki ili asali hiyo iweze kuingia kwenye masoko ya hapa nyumbani pamoja na nje ya nchi.
Lakini pia wananchi hao wameshauriwa kulinda na kuyatunza mazingira yanayowazunguka kwani kupanda miti pamoja na maua mbali mbali yanasaidia kupatikana asali kwa wingi hivyo kupata faida na manufaa katika soko la asali.
Pia wananchi hao wameweza kueleza kuwa changamoto kubwa wanazokutana nazo ni athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo ukame pamoja na changamoto ya ukosefu wa mbao za kutengenezea mizinga imara ya nyuki.
Mafunzo ya ufugaji nyuki wakubwa na wadogo yanatolewa kwa wananchi wa Wilaya ya Hai waliojiunga kwenye vikundi ili kuwaongea wigo kupata kipato cha kaya zao lakini pia ni namna bora ya kuimarisha untunzaji wa mazingira.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai