Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amefurahishwa na kuridhishwa na ujenzi wa barabara ya Nyerere yenye urefu wa km 0.79 kwa kiwango cha lami.
Barabara hiyo iliyogarimu kiasi cha shilingi milioni 429.32 imelenga kurahisisha usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa wilaya ya Hai hasa wa kata ya Bomang’ombe.
Akiweka jiwe la msingi wakati wa mbio za Mwenge 2023, Kaim amesema ameridhishwa ujenzi wa miradi huo unavyogusa mahitaji ya jamii husika huku viwango vyake vikiwa havina mashaka.
“Tarura wamefanya kazi nzuri na Mwenge wa Uhuru umejiridhisha na mradi, niombe tuendelee kuusimamia mradi huu na kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa”,amesema Kaim.
“Ninyi mnahitaji pongezi kwa viwango vilivyofanyika katika barabara hizi mnazojenga kwa kiwango cha lami, nataka wengine waje wajifunze kwenu maana hii ni alama ya mafanikio yenye tija kiuchumi”,amesisitiza.
Kwa upande wake Mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe ameishukuru serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kusema kuwa itasaidia kuboresha maisha ya wananchi wa hai na kufungua uchumi.
Saashisha amesema zipo barabara zaidi ya nne zinajengwa kwa kiwango cha lami huku akiitaja barabara ya Bomang’ombe kikavu chini itakayojengwa kwa kiwango
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai