Ulaji duni na ulishaji wa watoto na mtindo wa maisha usiofaa umetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa tatizo la utapiamlo nchini.
Hayo yamesemwa na afisa lishe wilaya ya Hai Bi katika maadhimisho ya siku ya lishe yaliyofanyika wilayani humu yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya kitongoji cha bondeni wilayani humo.
Amesema chi yetu inakabiliwa na matatizo makuu matatu ya kilishe yaani; Utapiamlo wa lishe pungufu, Utapiamlo wa upungufu wa madini na vitamini pamoja na Utapiamlo wa lishe ya kuzidi.
Nakuongeza kuwa takwimu za Kitaifa za Afya na Demografia nchini za mwaka 2023 zinaonesha asilimia 30 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wamedumaa, asilimia 12 wana uzito pungufu na asilimia 3 wana ukondefu. Ukilinganisha na takwimu za miaka mitano iliyopita tatizo la utapiamlo linapungua, kwa mfano kwa takwimu za mwaka 2023 zinaonesha kuwa, upungufu wa damu kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano ni asilimia 58.
Kwa upande wake mgeni rasm ambae ni mkuu wa wilaya hiyo Mh. Razaro Twange pamoja na kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na wahudumu wa afya wilayani humo hasa kitengo cha lishe amewasisitizia wananchi kubadilika na kurudi kutumia vyakula vya asili huku akisititiza kuwa nia njema ya rais wa jamuuri wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hasan ya kuleta maendeleo nchini inaweza kutimia iwapo tu jamii itakuwa na afya njema inayoperekea nguvu kazi kuongezeka
Maadhimisho ya Siku ya Lishe mwaka 2024 yaliongozwa na kaulimbiu inayosema “Mchongo ni Afya yako, Zingatia unachokula”. Kaulimbiu inayohimiza jamii kuchukua hatua ya makusudi ya kuwa makini na kufanya maamuzi sahihi kuhusu aina na ubora wa vyakula wanavyokula au kuwalisha watoto, ili kulinda afya zao kwa ustawi kamili kijamii na kiuchumi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai