Baadhi ya watoto wa kike katika familia za kifugaji hushindwa kufikia malengo yao ya kielimu kutokana na kutokukubali kutoa ushirikiano pale mzazi anapomshinikiza kukeketwa au kuolewa katika umri mdogo.
Akizungumza kwenye kipindi cha Siku mpya kinachorushwa na Redio Boma Hai fm, Afisa ustawi wa jamii wilaya ya Hai Helga Simon amesema ”mara nyingi hatuwezi kufanikiwa katika kesi mahakamani kwa sababu shahidi wa kwanza anakuwa ni yeye (Mtoto) ambaye anasema baba yake asifungwe wala hataki atajwe popote kisheria ila anataka tu yeye asome”
“Jambo ambalo tunalifanya ili kuhakikisha kwamba mtoto huyo anapata zile haki zake, tunashirikisha viongozi wa kijamii, viongozi wale wa mila, viongozi wa Serikali za kijiji tunawakabidhi mtoto yule asome chini ya uanglizi wao na wahakikishe kuwa anamaliza shule”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai