Wananchi wa Kijiji cha Kyuu kata ya Masama Magharibi wilayani Hai wameitaka jamii kuachana na ushirikina unaosababisha ukatii kwa watoto .
Wananchi hao wametoa wito huo wakati wa zoezi la utoaji wa Msaada wa kisheria lililofanyika katika Kijiji hicho ambalo limeambatana na utoaji wa elimu ya kisheria.
Wamesema imefika wakati sasa jamii ikabadilika na kuachana na taama ya kupata fedha za haraka hali inayochangia ongezeko la ukatili ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na ukatili kwa watoto.
“Tunasikia matukio mengi kupitia vyombo vya Habari ,kila kukicha unasikia tukio jipya tena la kusikitisha baba ana mlawiti mtoto wake wa kumzaa,ubakaji na ulawiti unaonegezeka kila siku.”
Wananchi hao pia wameiomba serikali kufanya uhakiki wa waganga wa jadi ambao baadhi yao wamekiuka masharti ya vibali vyao na wengine kufanya kazi bila vibali huku wakidanganya watu kuwa wana uwezo wa kuwapa utajiri.
“hivi mtu mzima amekosa mtu wa kumtimizia haja zake hadi ambake mtoto wa miaka miwili? Hii si akili ya kawaida ,ni ushirikina umetawala”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai