Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Hai Hussein Kitingi ameeleza kuwa mradi wa BOOST wilaya ya Hai imetokea fedha kiasi cha shilingi 949,100,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za Msingi, matundu ya vyoo pamoja na shule mpya kupitia mradi wa Boost.
Kitingi ameeleza hayo alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha baraza la mamlaka ya mji mdogo katika ukumbi wa Halmashauri hiyo na kusisitiza wanaotekeleza miradi hiyo wahakikishe kuwa inakamilika kwa wakati huku akiagiza usimamizi madhubuti uendelee.
"Fedha za mradi huu ni tekeleza kwa matokeo ambapo sasa ili tupate zaidi maana yake ni kwamba awamu hii ya kwanza tufanye kwa mafanikio zaidi, mafanikio yenyewe ni pamoja na ubora, lakini sambamba na hilo kukamilika kwa wakati.
"Naomba katika maeneo yetu tukaongeze usimamizi wa miradi ikamilike kwa wakati ili mwisho wa siku tupate miradi mingine" aliongeza Kitingi kuhusu miradi ya BOOST
Shule zilizopokea fedha za mradi wa BOOST zilizotolewa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni pamoja na shule mpya eneo la Mlima shabaha 348,500,000, shule ya msingi Narumu, 144,100,000, shule ya msingi Kingereka 106,300,000.
Shule nyingine zilizopokea fedha hizo ni pamoja na shule ya msingi Kawaya Kati, 106,300,000, shule ya msingi Kikavu chini 106,300,000, shule ya msingi Mkalama 106,300,000 pamoja na shule ya msingi Msamadi 31,300,000.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai