Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Abdllah Shem Kaim ameridhishwa na hatua ya serikali kutunza vyanzo vya maji pamoja na mazingira ya chanzo cha maji Njoro ya blue katika kata ya Masama Rundugai wilayani Hai.
Akizungumza wakati wa kukagua maradi wa uoteshaji miti na utunzaji wa mazingira katika chanzo hicho Kaim amesema kwa kuhifadhi mazingira hayo ni kuungana na kauli mbiu yam bio za Mwenge 2023 unaosema “Tunza mazingira ,Okoa vyanzo vya Maji Kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.
“Ni katika kutekeleza agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na khifadhi mazingira yetu sambamba na kuhifadhi vyanzo vya maji, kama haitoshi ndugu zangu kazi kubwa iliyofanyika ni kuunga mkono kauli mbiu ya Mbio za Mwenge mwaka huu unaosisitiza juu ya mabadiliko ya tabia nchi hifadhi ya mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya maji Bonde la mto pangani Mhandisi Segule Segule amesema katika chanzo hicho wamejidhatiti kwa kuweka mabango ya makatazo kwa jukumu hilo linapaswa kufanywa na bodi hiyo.
Mradi huo wenye gharama ya shilingi 15,880,000 umelenga kuhifadhi mazingira ya eneo hilo na kuwezesha kilimo cha umwagiliaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai