Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Bi Happiness Eliufoo ametoa shukrani kwa viongozi wa Serikali kwa jitiada za kuunga mkono miradi inayofanywa na wanawake wilayani Hai.
Akitoa shukrani hizo i kwa niaba ya wanawake wa wilaya ya Hai mbele ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mh. Ummy Nderiananga wakati wa kutembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo amesema kuwa wanawake wilayani Hai wanatambua mchango mkubwa unaofanywa na viongozi wa serikali hasa katika kuwakwamua kiuchumi.
"Mh Naibu waziri nikushukuru sana kwaniaba ya wanawake wote wa wilaya ya Hai na pia tufikishie salamu zetu kwa Rais Samia, sisi wanawake wa wilaya ya Hai tunaziona juhudu za moyo wa dhati kutoka kwa Rais na serikali anayoiongoza na hata wewe kufika hapa ni kututhamini wanawake" Alisema Happyness.
Katika ziara hiyo ya siku moja wilayani Hai Mh Ummy Nderiananga alikagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa jengo la kina mama wa UWT pamoja na ujenzi wa zahanati unaoendelea katika Kijiji cha kimashuku kata ya Mnadani, ambapo alitoa pongezi za dhati huku akiwataka wanawake kuzidi kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni njia sahihi ya kumuunga mkono Rais Samia.
Naibu waziri Mh.Ummy Nderiananga alichangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati pamoja na tofali 500 kwa ajili ya jengo la UWT.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai