Serikali mkoani Kilimanjaro imedhamiria kutoa vyeti vya ufundi kwa wanafunzi wote waliorasimishwa ujuzi ikiwemo mafundi vijana waliopata ujuzi mtaani baada ya kumaliza mafumzo yao na kuwasaidia kuajiliwa kwenye taasisi mbalimbali.
Akizungumza na mafundi vijana katika semina ya urasimishaji ujuzi wa vijana walio nje ya mfumo wa elimu ya ufundi Mwalimu Evance Moshiro amesema Serikali imedhamiria kuwarudisha vijana hao katika mfumo rasmi.
Aidha amesema baada ya kuwepo kwa mwitikio mzuri wa vijana hao umewekwa mpango wa kuwapatia vyeti vitakavyowasaidia kuingia katika ushindani wa ajira huku kukiwapo na utofauti kati yao na waliosajiliwa na kusoma VETA katika mfumo rasmi wa miaka 3.
Kwa upande wao wanafunzi wameshukuru sana Serikali ya awamu ya tano kwa kutambua uwepo wa vijana waliopo mtaani lakini hawana vyeti na kukosa namna ya kuanza kutafuta ajira kupitia ufundi wao na kuwasihi vijana wengine waendelee kupambana na kuongeza bidii katika kazi zao.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Vijana wilaya ya Hai Lucila Chima ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa namna inavyojali vijana na kuwataka wajitokeze kwa wingi pale fursa hii itakapojirudia na kuwaomba waliobahatika kupata mafunzo hayo kuwa mabalozi mitaani ili pasiwepo na kijana asie na kazi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai