Zaidi ya vijana 4500 wa wilaya ya Hai wanatarajiwa kunufaika na mradi wa Vijana (Enhancing Livelihood Prospects for Young People) utakaotekelezwa katika wilaya nne mkoani Kilimanjaro ikiwemo wilaya ya Hai.
Akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi huo Winnie Muine ambaye ni Meneja wa Mradi Kutoka DSW amesema mradi huo utakaohusisha wadau watatu HRNS Tanzania, Khune Foundation, DSW Tanzania umelenga kuwawezesha Vijana kuboresha maisha yao katika maeneo ya Afya, Elimu, kipato pamoja na ustawi wao kwa ujumla ili waweze kufikia malengo yao.
Ameendelea kwa kusema mradi huo unatekelezwa katika Mikoa minne ukiwemo mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na Songwe kwa muda wa miaka minne ( 2023-2027) unaotarajiwa kunufaisha vijana takribani 50,000 ambapo kwa Mkoa wa Kilimanjaro utatekelezwa katika wilaya ya Rombo, Siha, Moshi vijijini pamoja na Hai.
Akizungumza katika zoezi hilo la utambulisho wa mradi huo Afisa Rasilimali watu Mkoa wa Kilimanjaro ndugu Amos Machilika amewataka wadau kuendelea kufanya kazi karibu na serikali katika kuhakikisha wanajua vipaumbele vya serikali hususani katika Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na fursa zilizopo serikalini.
Katika utekelezaji wa mradi huo kila shirika lina jukumu lake ambapo HRNS Tanzania watajikita zaidi na masuala ya kuwawezesha vijana wa kike na kiume katika Sekta ya Kilimo, Khune Foundation watajikita zaidi katika kutoa fursa za Elimu ya Juu na Vyuo vya ufundi katika maeneo ya uratibu, usafirishaji, na ugavi na DSW Tanzania watajikita katika Elimu ya Stadi za Maisha, Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Elimu ya Afya ya Uzazi pamoja na utumiaji na upatikanaji wa Huduma Rafiki kwa Vijana.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai