Wito umetolewa kwa vikundi vya kijasiliamali wilayani Hai mkoani kilimanjaro kuhakikisha wanafanya marejesho ya fedha za asilimia 10 za halmashauri kwa wakati ili vikundi vingine vinufaike na kuepuka adha ya kufunguliwa mashtaka au kufikiswa mahakamani.
Hayo yamesemwa na mwanasheria wa Halmashauri hiyo Blandina Mweta kwenye mafunzo kwa vikundi vinavyotarajia kupokea mkopo ili kuvipa mbinu bora usimamizi wa fedha uendelezaji wa miradi ili viweze kunufaika na mikopo hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa idara ya maji bomang’ombe.
“Kwa mfano Kuna vikundi vinakuja kuomba mkopo lakini vikitoka hapo havifanyi ile kazi iliyokusudiwa wanaishia kugawana fedha hizo na mwisho wa siku wanashidwa kurejesha mkopo sisi kama Halmashauri tukigundua watu kama hao tutawachukulia hatua Kwakutoa taarifa za uongo maana sio kikundi”
Aidha amesisitiza kuwa ni vema vikundi vitoe taarifa kwa wakati pale wanapopata changamoto katika kutekeleza majukumu yao kwani halmashauri ina wataalamu wengi watakao washauri namna bora ya kutimiza malengo yao na kudokeza kuwa kuna vikundi ambavyo vimeshafikishwa mahakamani kwa makosa kama hayo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai