Vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wamesisitiziwa kuweka Akiba itokanayo na faida ya biashara wanazofanya.
Akizungumza wakati wa Kutoa mafunzo Kwa vikundi hivyo vinavyotarajiwa kupewa mkopo utokanao na asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri, afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Hai Elia Kapinga amesema umuhimu wa kuweka akiba kwa wana kikundi ni pamoja na kukabiliana na dharura, kuwezesha miradi ya Maendeleo na kuongeza uwekezaji.
Kapinga ametaja faida zingine ni kujenga Umoja na ushirikiano katika kikundi,kuwezesha kuwahi fursa na kuongeza nidhamu ya matumizi ya fedha.
Amesema pamoja na faida hizo, athari zitokanazo na kutoweka akiba ya vikundi ni kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na dharura,kukwama kwenye Maendeleo, kuongezeka kwa utegemezi wa kikundi na kukosa fursa za uwekezaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai