Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Lazaro Twange ametoa wito kwa vikundi vilivyopewa Mkopo wa serikali wa asilimia 10 unaotokana na mapatao ya ndani ya Halmashauri usio na riba na kutumia mikopo hiyo kufanya kazi Kwa bidii ili kukuza biashara na kuongeza kipato.
Ameyasema hayo Leo Novemba 19,2024 wakati akitoa mikopo hiyo kwenye vikundi 20 vya akina mama,vijana na watu wenye ulemavu yenye jumla ya shilingi 198,437,000/=. Akiwataka kujihusisha na shughuli za kiuchumi kama kilimo, ufugaji, biashara ufundi na kuongeza thamani ya mazao.
Aidha Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe.Saashisha mafuwe amewaasa wanavikundi wote ambao wamepokea mikopo na ambao hawajakidhi vigezo waungane kwa pamoja na kuona juhudi za Serikali katika kuinua uchumi wa wananchi wake.
Vile vile amewataka wananchi wote kujitokeza kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tarehe 27 Novemba 2024 ili kuchagua viongozi wazuri watakaoleta maendeleo kwa maslahi ya wananchi wote.
Nae Afisa maendeleo ya jamiiii ndugu Robert Mwanga akitoa taarifa ya mikopo inayotolewa amesema kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambapo vikundi 14 vya wanawake vinakopeshwa shilingi 139,142,000 vikundi viwili vya vijana shilingi 36,211,000 na vikundi 4 vya watu wenye ulemavu shilingi 23,084,000 na katika robo ya pili Octoba Hadi Decemba 2024 halmashauri inatarajia kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi 364,567,257,37 kwenye vikundi vitakavyokidhi vigezo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai