Watendaji wa Serikali mkoani Kilimanjaro wametakiwa kutimiza wajibu wao kwa weledi na uaminifu katika kupunguza kero na shida zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwenye ufunguzi wa mafunzo ya viongozi hao katika masuala ya kusajili watoto; Mkuu wa Wilaya ya Siha Onesmo Buswelu amesema ni lazima kila mtendaji atambue na kutimiza wajibu wake ili kwa pamoja kuchangia maendeleo ya Taifa.
Amewataka viongozi hao kuwahamasisha wazazi kuchangamkia fursa ya kuwasajili watoto wao ili wawe na nyaraka stahiki za utambulisho wao lakini pia kusaidia mamlaka za usajili kuwa na takwimu sahihi za wananchi waliosajiliwa.
Aidha Buswelu amewakumbusha mamlaka ya RITA kuhudumia watendaji wao waliopo kwenye ngazi za wilaya ili kuwasaidia kufanikisha majukumu yao kwa ufanisi ikiwemo kuwasaidia kufikia maeneo ya vijijini kutoa elimu na huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Kaimu Kabidhi Washi Mkuu wa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson amesema mkutano huo umelenga kuwajengea uwezo viongozi wakuu katika Mkoa wa Kilimanjaro kuhusu usajili wa watoto chini ya miaka mitano ili wakati wa kutekeleza zoezi hilo viongozi hao wawe na uelewa na pia kusaidia ufanisi wa zoezi husika kila mmoja kwa nafasi yake.
Amesema usajili wa watoto ni zoezi muhimu kwani watoto wanatambulika na kuweza kupata huduma wanazohitaji kama za afya, elimu na nyingine huku serikali ikitumia takwimu za idadi ya watu katika kupanga namna bora ya kuhudumia watu wake ikiwemo kupanga mipango ya maendeleo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai