Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya amezitaka taasisi mbalimbali kushiriki kikamilifu zoezi la utolewaji wa chanjo ya surua na rubela kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano linalotarajiwa kuanza Oktoba 17 mwaka huu.
Taasisi hizo ambazo Ole Sabaya amezitaka kushiriki kikamilifu zoezi hilo ni pamoja na zile za dini kuhakikisha kuwa zinatoa elimu kwa waumini wao juu ya umuhimu wa kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo na kuepuka magonjwa yanayokingika kwa chanjo.
Akizungumza leo katika kikao cha kamati ya afya ya msingi wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa afya na kusisitiza kuwa chanjo ni zoezi la kitaifa na hafungamani na imani zozote za dini wala kabila hivyo jamii nzima inapaswa kushiriki kikamilifu na kumuagiza mganga mkuu wa wilaya kuwaandikia barua maafisa wote wa afya kata kuhakikisha kuwa sababu zinazopelekea ueneaji wa ugonjwa huo zinapungua au kutoweka kabisa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo ameagiza kamati za afya za vijiji kulichukulia jambo hili kama ajenda kuu katika utendaji wao na kwenye vikao vyote vya vijiji wanavyohudhuria kwa kuwa wapo karibu zaidi na jamii.
Akichangia katika mkuatano huo, katibu tawala wilaya ya Hai Upendo Wela amesema kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa sana yakuhamasisha jamii katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwani jamii inawaamini lakini pia ametaka jamii kuhamasishana kwa kuwa zoezi la chanjo ni muhimu katika maisha yao wenyewe.
Awali akitoa taarifa ya kampeni hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai Dk. Irene Haule amesema zoezi hilo kitaifa na kiwilaya litazinduliwa Octoba 17, mwaka huu ambapo litafanyika kwa siku tano lengo kuu ni kuwafikia watoto wa miaka mine na miezi 59 wapatao 28,911 na watoto 16,100 zoezi watakaopata chanjo ya surua ya sindano.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai