SERIKALI wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, imegiza viongozi wa vijiji pamoja na wananchi kuhakikisha kuwa wanatunza miti inayooteshwa ili kuboresha mazingira pamoja na kukabiliana na ukame katika maeneo mbalimbali.
Agizo hilo limetolewa kwa nyakati tofauti na Katibu tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wella kwa niaba ya mkuu wa Wilaya Juma Irando, katika zoezi la upandaji miti kwenye wiki ya maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru Tanganyika.
Amesema kuwa zoezi la kupanda miti limekuwa likifanywa kila mara la jamii imekuwa ikipanda kwa ajili ya maadhimisho na kusahau jukumu la kuitunza jambo ambalo limesababisha kuendelea kuwa na mazingira ya ukame.
Amesema kuwa kutokana na wananchi kupanda miti pasipo kuitunza kunafanya nchi kuendelea kuwa jangwa pamoja na kusababisha vyanzo vya maji kukauka na mazingira ya maeneo ya makazi kutokuwa bora.
Amefafanua kuwa miti iliyooteshwa inatunzwa na haikatwi hovyo, na kwambi hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakaye kata miti hovyo pasipo kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali
Kwa upande wake Afisa Maliasili Wilaya ya Hai, Mbayani Mollel amewakumbusha viongozi wa vijiji kitunza na kuilinda miti iliyooteshwa ambayo itasaidia kutunza mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadaye huku akiahidi kuwapa ushirikiano pale watakapohitaji msaada wa kitaalamu katika utunzaji wa mazingira.
Maadhimisho ya miaka 61 wilaya Hai yamefanyika kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi ,kuotesha miti 300 kwenye Vituo vya Afya vya Chekimaji na Longoi .
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai