Mkuu wa wilaya ya hai Juma Saidi Irando amewataka wafugaji,wakulima na wanachi wote wa kijiji cha longoi kata ya Weru Weru wilayani Hai kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji katika kata hiyo ili kuendelea kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo ameyasema katika ziara yake aliyoifanya January 11, 2023 katika katika kata hiyo ya Weru Weru kwenye ofisi ya kijiji cha Longoi wakati akisikiliza changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi wa kata hiyo na kuzitolea ufafanuzi.
Aidha Irando amewataka viongozi wa kata na vijiji kuweka utaratibu wa kukutana na wafugaji pamoja na wakulima na kuzungumza nao ili kuweza kuondoa migogoro na changamoto zilizopo baina yao hali inayosababisha kutokuelewana.
Hata hivyo amewataka viongozi hao pindi wanapokutana na wafugaji kupata idadi ya mifugo kwa kila mfugaji na kuweka utaratibu wa wapi mifugo ikae na wapi mifugo isikae ili kuepuka uharibifu wa vyanzo maji katika maeneo yao.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai