Mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa amewapongeza viongozi wa vyama vya ushirikia wilayani humo kwa kuratibu na kusimamia vema mashamba na vyama vyao na kuhakikisha kuwa wahusika wote wananufaika .
Mkalipa ametoa pongezi hizo mapema leo Aprili 14 wakati wa kikao na viongozi wa ushirikia wilayani humo kilicholenga kujitambulisha kwao na kusikiliza kero na changamoto zinazo kabili vyama hivyo.
"ninazo taarifa ofisini kwangu ,kwamba mmechangia kwenye ujenzi wa sehemu za kutolea uduma ya afya na huduma ya shule katika vijiji vyenu, taasisi zenu kama sio bodi zenu zimetumika kuichangia serikali katika kuwaletea wanachi maendeleo lazima tuwapongeze kwa uhamuzi wa busara hongereni sana"
Pamoja na pongezi hizo Mkalipa amevitaka vyama vya ushirika kuzingatia taratibu zote za ushirika hasa katika suala la matumizi ya fedha za ushirika kwakuwa fedha hizo sio zao binafsi bali ni za Umma.
Amesema fedha za ushirika ni lazima zifuate taraibu zote za Umma na ndio maana vyama hivyo ukaguliwa kila mara na maafisa usharika na inapo bainika kuna matumizi mabaya ya fedha hatua uchukuliwa na mrajisi.
'kuna watu wanadhani kuwa ushirika sio serikali, ushirika ni serikali tukikupa shamba haina maana kuwa ni mali ya bodi, ni mali ya serikali iliyo chini ya dhamana ya ushirika na ndio maana endapo chama au bodi haitofuata sheria watakakuwa wamepoteza haki ya kumiliki shamba hilo na litarudi kwa serikali".
Mbali na kusisitia juu ya matumizi ya fedha yanayofuata taratibu za serikali , Mkuu wa Wilaya pia amesisitiza juu ya vyama hivyo kufanya uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa taratibu na sheria ya ushirika nchini.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai