Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amewataka viongozi wa Dini na Viongozi wa Serikali kuendelea kutoa elimu pamoja na kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika kuanzia Agost 23 mwaka huu.
Babu ameyasema hayo Agost 17 katika hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Stephen Kagaigai.
Amesema kuwa ni lazima kuhamasisha ili kila Mwanachi wa Kilimanjaro afahamu umuhimu wa kuhesabiwa na kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa kwani kuhesabiwa kutaifanya serikali kupanga mipnago ya Maendeleo kutokana na Takwimu sahihi za watu.
Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa Mkoa Kagaigai ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya TBC Taifa amewashukuru wananchi wa Kilimanjaro,viongozi wa Dini pamoja na watumishi wote kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichokuwa mkuu wa Mkoa na kuwataka kumpa ushirikinao Babu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai