Madiwani pamoja na watendaji wa kata na vijiji Halmashauri ya wilaya ya Hai wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano ili kuwezesha utekelezaji wa zoezi la anwani za makazi kwenye maeneo yao ili zoezi hilo likamilike kwa wakati kulingana na mpango wa serikali.
Hayo yamesemwa Marchi 21 2022 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Edmund Rutaraka wakati akizungumza katika kikao kilichowakutanisha madiwani pamoja na watendaji wa kata na vijiji lengo likiwa ni kujadili mwenendo wa zoezi la uandikishaji wa anwani za makazi ambalo linaendelea ndani ya wilaya ya Hai.
Katika kikao hicho mwenyekiti wa Halmashauri amemtaka Kaimu mkurugenzi kufanyia kazi changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na madiwani wakati wa kikao hicho ikiwemo suala la malipo kwa wenyeviti wa vitongoji ambao ndio wanaosimamia kwa ukaribu suala hilo.
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Rajabu Yateri amesema wao kama Halmashauri wamezipokea changamoto mbalimbali ambazo zimebainishwa na madiwani hao na kuahidi kuzifanyia kazi ili kufanikisha utekelezaji wa zoezi hilo kwa ufanisi.
Miongoni mwa hoja zilizoibuliwa na madiwani katika kikao hicho ni pamoja na kutaka kuwepo kwa vitambulisho kwa wale wanaofanya zoezi hilo la uandikishaji ili waweze kutambulika na kupata ushirikiano wanapofika sehemu husika.
Zoezi la uandikishaji wa anwani za makazi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai limeanza kutekelezwa marchi 18 2022 na linatarajiwa kukamilika Aprili 1, 2022.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai