Vitongoji 18 kati ya 19 ambavyo havina umeme wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro vinatarajiwa kuwekewa umeme hivi karibuni.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa katika mkutano wa baraza la madiwani robo ya nne 2023/2024 ambapo amesema kuwa vijiji vyote katika wilaya ya Hai vimefikiwa na umeme isipokuwa vitongoji 19 tu.
Mkalipa amesema kwa sasa vitongoji 13 vina umeme pungufu na vitongoji 19 havina umeme kabisa na kwamba serikali imejipanga kuhakikisha kuwa vitongoji vyote vinapata umeme toshelezi.
Akizungumzia hali ya upatikanaji wa maji amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 900 Kwa ajili ya kuendelea kuboresha mradi wa Maji ili kuhakikisha kuwa maeneo yote yanaendelea kupata Maji ya kutosha.
Katika hatua nyingine amewataka wananchi na viongozi wa wilaya ya Hai kujiaandaa vyema na uchaguzi ujao na kusema kuwa kama wilaya wamejipanga vizuri na uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai