Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Julius Mduma amewataka wajumbe wa mazingira kuzingatia hatua zote muhimu za utunzaji wa miti ili kuleta mabadiliko mazuri na kutunza uoto wa asili.
Ameyasema hayo leo Mei 10 2022 wakati akifungua semina ya mafunzo ya utunzaji miti iliyohusisha, walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na idara ya maliasili na utalii, iliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mduma amewataka wajumbe hao kuendelea kuchimba mashimo ya kuoteshea miti huku akiwaahidi kuwa changamoto wanazokabiliana nazo zitaendelea kufanyiwa kazi.
Naye Mkurugenzi wa Kijani Pamoja Fredrick Marealle amehaidi kuendelea kufanya ufuatiliaji wa kitafiti wa miti hiyo pindi itakopo oteshwa huku akisisitiza upandaji wa miti ya asili inayoendana na mazingira ya eneo husika
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo amesema kuwa utunzaji wa miti hiyo utaleta faida ya fedha kiasi cha shillingi mia nne [400] kwa kila mti baada ya miezi mitatu [3] na kuwaomba watumie fursa hiyo kuotesha miti na kuitunza ili wawaze kupata kipato hicho.
Hata hivyo halmashauri kushirikiana na wajumbe kutoka sekta binafsi na serikali wanategemea kuotesha miti Zaidi ya elfu hamsini[50000]
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai