Wafanyabiashara wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuacha kupandisha bei ya sukari kwa madai kuwa imeadimika na badala yake wafuate bei elekezi iliyotangazwa na serikali.
Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la kukagua maduka yaliyopandisha bei ya sukari na kubaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara waliokiuka maagiza ya serikali na kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu
“Serikali imeshatoa bei elekezi ya sukari kwa kila mkoa na hapa mkoani kwetu sukari itauzwa kwa bei ya rejareja kwa shilingi 2700 kwa kilo na sio vingine ”amesema Sabaya
“Katika ukaguzi wangu leo nimekuta maduka yanauza sukari kati ya shilingi 3000 na 3500 kwa kilo jambo hili stalivumia kabisa kuona wananchi wakidhulumiwa kwa kuuziwa sukari kwa Bei ya juu angali serikali imeshatoa maelekezo ”amesisitiza
Ameongeza “Waziri wa viwanda na biashara amepiga marufuku upandishaji wa bei , Waziri mkuu amesha sema sukari nchini iko ya kutosha iweje ninyi wafanyabiashara mpandishe bei na kushindwa kufuata maelekezo yanayotolewa , Serikali wilayani hapa haitamvumilia yeyote atakayekiuka agizo la serikali”
Ole Sabaya amesema wafanyabisha waache kutumia mwezi huu mtukufu wa Ramadhani pamoja kupandisha bei ya bidhaa na badala ake watumie muda mwingi kumwomba Mungu ili kuepusha na Janga hili la Corona linaloendelea kushika kasi nchini.
Kwa upande wake Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilayani Hai , Ernest Muhapa amesema kuwa wataendelea kufuatilia maagizo ya serikali ya ukomo wa bei za bidhaa ili wananchi waendelee kupata huduma kwa unafuu.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia zoezi hilo la ukaguzi wa bei ya sukari wamepongeza hatua ya serikali kutoa bei elekezi hali ambayo itasaidia kupunguza ukali wa maisha
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai