Jumla ya wagombea 123 wa Chama cha mapinduzi CCM katika vitongoji na vijiji wanaoshiriki wa serikali za mitaa wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wamepita bila kupingwa baada ya wagombea wa vyama vya upinzani kushindwa kujitokeza kuchukua na kurejesha fomu za ugombea.
Taarifa hiyo imetolewa leo na msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Bw.Juma Masatu.
Masatu amesema kuwa baada ya kukamilika kwa zoezi la urejeshaji fomu kwa wagombea Novemba 4 mwaka huu ,wagombea wa upinzani katika vitongoji 294 baadhi yao hawakujitokeza kuchukua fomu na kupelekea wagombea 110 wa CCM katika vitongoji hivyo, kupita bila kupingwa huku katika vijiji 62 wagombea 13 CCM wakipita bila kupingwa kutokana na wagombea wa vyama vya upinzani kushindwa kuchukua fomu.
Aidha amesema kuwa hatua inayoendelea hivi sasa nikubandika majina ya wagombea wenye sifa na wasio na sifa ya kugombea kutoka kila chama cha siasa kwa vitongoji na vijiji vyote na majina hayo yatabandikwa kwenye mbao za ofisi za vijiji na kuwataka wananchi kujitokeza kwenda kuangalia majina ya wenye sifa ya kugombea kwenye vijiji na vitongoji vyao ambapo itatoa fursa ya kuweka pingamizi kwa asiye nasifa.
Ameongeza kuwa Pingamizi linatakiwa kuwekwa na mgombea dhidi ya mgombea mwingine na mapingamizi hayo yanapokelewa ofisini kwa msimamimizi wa uchaguzi Novemba 5 hadi Novemba 6 mwaka huu.
Kwa mujibu wa kanunu za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa za mwaka 2019 inaeleza kuwa mtu yoyote anaekusudia kugombea na fasi ya uenyekiti wa kijiji, ujumbe wa halmashauri ya kijiji au uenyekiti wa kitongoji atatakiwa kuchukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi husika siku zisizo pungua 26 kabla ya siku ya uchaguzi kwa kadiri itakavyoelekezwa na msimamizi wa uchaguzi.
Uchaguzi huo wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika kote nchini novemba 24 mwaka huu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai