Kamati ya lishe Wilaya ya Hai imeshauri wajasiriamali wanaotengengeneza bidhaa za chakula, dawa na vipodozi na kuviuza kwa wananchi bila kufuata taratibu kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
Akizungumza katika kikao cha kamati hiyo, kaimu Mkurugenzi ndugu Elia Machange amewataka wajasiriamali hao kuwasiliana na ofisi ya mganaga mkuu wilaya ili kupewa utaratibu wa kuwezesha bidhaa zao kupimwa na mamlaka husika ili kuthibitisha ubora.
Kwa upande wake afisa afya ndugu Fredy Kaduma amesema bidhaa za vyakula,dawa na vipodozi ni muhimu kukaguliwa na kupimwa kabla ya kuanza kutumiwa na wananchi ili kulinda usalama wa mtumiaji.
Amesema baadhi ya wananchi wanaweza kuathirika kwa kutumia bidhaa hizo ambazo wakati mwingine madhara yake hayaonekani kwa haraka na hivyo kumfanaya hata mtumiaji kushindwa kujua chanzo cha tatizo lake.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai