Viongozi wa kata na vijiji katika kata ya Masama Rundugai wametakiwa kuwajibika kwa wananchi ili kuepusha maswali na sintofahamu kwa wananchi hao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Hai Juma Said Irando January 10, 2023 alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mkutano na wanachi hao lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata hiyo.
“Viongozi wa vijiji vya Rundugai watendaji embu jaribuni kuwajibika tunatakiwa kuwajibika kwa wananchi hawa,Mwenyekiti hapa wewe ulichaguliwa na wananchi,Mh diwani wewe ulichaguliwa na wananchi embu tuwahudumie tufanye kazi yetu angalau kwa asilimia 70 yaani kama wote wangekuwa wanafanya vile inavyotakiwa aya maswali yasingekuwa mengi”
Aidha Irando amewataka wenyeviti wa vijiji vitongoji kuwasomea wananchi mapato na matumizi kwani ni muhimu wananchi kujua ili kuepusha migogoro kati ya wananchi na viongozi.
“Itisheni mkutano na wasomeeni wananchi mapato na matumizi,katika vitu ambavyo vimekuwa changamoto kwa wenyeviti wengi ni kutowasomea wananchi mapato na matumizi hivyo hakikisheni mnafanya hivyo”
Kwa upande mwingine Irando amemuagiza Mtendaji wa Halmashauri kutenga sehemu kwa ajili ya wafugaji ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji huku akiwataka wafugaji kujifunza nakuwa na ushirikiano mzuri na wakulima na yeyote atakayekwenda tofauti sheria kali zitachukuliwa dhidi yake.
“Wafugaji wajifunze namna ya kuishi na wenzao wakulima haiwezekani kila wakati wafugaji tu,wao hawapo juu ya sheria wajifunze na wakiendelea kukaidi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao”
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Dionis Myinga amesisitiza viongozi wa kata,vijiji na vitongoji kuwajibika zaidi kwani kuna mambo wangeweza yatatua wao bila kungoja viongozi wa wilaya kuja kuyatatua.
Diwani wa Kata ya Masama Rundugai Aziz Simbano amempongeza mkuu wa wilaya ya Hai na serikali inayoongozwa na Raisi Dr.Samia Suluh Hassani kwa miradi iliyoletwa kwenye kata yake na kuahidi kuipokea na kuisimamia miradi hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai