Wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa miradi ya miundombinu ya Barabara Wilayani Hai wameagizwa kukamilisha mirada hio kwa wakati.
Hayo yamesemwa Mei 8, 2023 na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai Mhe. Wang’uba Maganda pamoja na kamati ya Siasa ya Chama hicho Wilaya ya Hai wakiwa katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 kwenye miradi mbalimbali walitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Meneja wa wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) juu ya ujenzi wa barabara ya Nyerere na Bomang’ombe-Kikavu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya TARURA inaonesha kuwa ujenzi wa barabara ya Bomang’ombe-Kikavu Chini utakamilka tarehe 25/08/2023 huku barabara ya Nyerere ulitegemewa kukamilika 26/02/2023 muda ambao umeisha na kwa sasa ameongezewa muda wa nyongeza.
“Kwahio unatuambia tarehe 31 Mwezi huu hatutakuona kwenye Site”? Aliuliza Maganda kwa Mkandarasi BUILDERS AND LIME WORKS LTD anayenga barabara ya Nyerere.
Kutokana na hali Maganda amewasisitiza wakandarasi wote wanaofanya kazi katika wilaya ya Hai kuhakikisha kuwa wanakamilisha miradi kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo kama ambavyo Serikali imekusudia Awali akitoa taarifa mbele ya Kamati hiyo Meneja wa TARURA wilaya Kuya Francis alisema awali Wilaya ya Hai ilikuwa na Bajeti ya takribani bilioni moja lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan aliongeza kiasi cha shilingi bilioni 4.5 na hivyo kufanya bajeti hiyo kufikia bilioni 5.5.
Ameongeza kwakusema kuwa ujenzi wa barabara ya Bomang’ombe-kikavu Chini kwa kiwango cha lami yenye urefu wa 0.5 km unaogharimu kiasi cha shilingi 299,00,000 barabara Nyerere yenye urefu wa 0.79 unaogharimu kiasi cha shilingi 418,225,000 ni sehemu ya miradi iliyotekelezwa kwa fedha hizo. Aidha Fraincis alisema lengo la miradi hiyo ni kuwezesha huduma za usafiri na usafirishaji, kuboresha mandhari ya mji, kuchochea shughuli za kiuchumi pamoja na kupunguza gharama za matengenezo ya barabara mara kwa mara.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai