• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Hai District Council
Hai District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hai

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Ardhi na Maliasili
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Taarifa Idara ya Kilimo
      • Mifugo na Uvuvi
        • Wasilisho Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
      • Maporomoko ya Maji ya Nshara
      • Chemchemi ya Chemka
      • Mila na Utamaduni
      • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Industry and Trade
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Kilimo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Mipya
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
      • Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi
      • Ahadi ya Uadilifu Watumishi
      • Fomu ya Maombi ya Likizo
      • OPRAS Walimu
      • OPRAS Watumishi
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Taarifa kwa Umma-Mikopo
    • Jarida
  • Mifumo
    • Mfumo wa Kiuhasibu (FFARS)
    • Mfumo wa Bajeti (Planrep)
    • Mfumo wa Vibali Safari za Nje
    • Mfumo wa Taarifa za Mapato (LGRCD)
    • Mfumo wa Taarifa za Shule (TanzaniaSIS)
    • Usajili Kupata TIN (TRA)

Wakandarasi Watakiwa Kukamilisha Kazi Kwa Wakati

Imetumwa: February 16th, 2022

MKUU wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Juma Irando  amewataka Wakandarasi waliopata  kazi za wakala wa barabara za Vijini  na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanazingatia mikataba yao na kusisitiza kuwa Serikali haitakuwa tayari kuona mikataba inapita muda wake wa utekelezaji na kutekeleza miradi hiyo kwa viwango na ufanisi unaotakiwa ili kuendana na thamani ya fedha.

Irando alitoa angalizo  hilo wakati akikagua  miradi ya matengenezo ya barabara inayotekelezwa  na (TARURA).

Amesema serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji barabara, hivyo ni lazima wakandarasi kufuata mikataba yao kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha.

“Sote tunafahamu umuhimu wa Sekta ya Barabara ni kiungo muhimu cha uchumi wa wananchi wetu. TARURA Mmepewa sekta nyeti ya kuchangia uchumi katika nchi yetu, tunahitaji kuona kasi.

“Katika maeneo machache ambayo hayafanyi vizuri tuongeze nguvu ya kusimamia kwa ukaribu zaidi ili wananchi waliotupa dhamana hii waweze kuona malengo ya uanzishwaji wa TARURA yanaendana na dhamira ya Rais wetu.”

Hata hivyo mkuu huyo wa Wilaya amemtaka Meneja wa TARURA wilaya hiyo, Mhandisi Rickson Lema  kuhakikisha kila mradi wa barabara unaosainiwa utekelezwe ndani ya kipindi cha mkataba, na kuongeza kuwa hatokubaliana na utaratibu wa kuongeza muda wa mikataba kwa Wakandarasi kama hakuna sababu za msingi.

Zaidi alisisitiza: “Kumekuwa na changamoto ya mikataba kutotekelezwa kwa wakati, mikataba inasainiwa lakini haimaliziki kwa wakati, hivyo tunalazimika kuongeza muda wa utekelezaji wake jambo ambalo linaongeza gharama, linapunguza thamani ya fedha na kupunguza ufanisi wa malengo ya Serikali, hivyo basi ni vyema mikataba yote ya ujenzi wa barabara ikazingatia masharti yaliyopo kwenye mikataba ili kuondoa changamoto hii.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Hai, Dionis Myinga amewataka wakandarasi hao kuhakikisha kuwa wanakamilisha miradi hiyo mapema kulingana na mikataba yao na kutokuwa na sababu kwa baadhi ya wakandarasi kutafuta sababu za hali ya hewa pindi wanaposhindwa kukamilisha kwa wakati .

Nae Meneja wa TARURA Rickson Lema alisema Serikali kwa mwaka wa fedha 2021 /2022 inatekeleza miradi 8 ya matengenezo ya barabara yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.5 zinatumika kutengeneza kwa kiwango cha changarawe, kujenga makalavati pamoja na kujenga mifereji kwa maji yasiweze kuharibu miundo mbinu hiyo pindi mvua zinaponyesha .

Amefafanua kuwa baadhi ya barabara kazi zinaendelea huku nyingine zikiwa zimekamilika ambapo amesema kuwa barabara ya Makoa Darajani hadi Mferejini  yenye urefu km 18.25 amesema kazi inaendelea kwa kufyeka na kuondoa vichaka vilivyopo eneo la barabara ili kupata upana unaotakiwa pamoja na kukata ngema na kutanua barabara eneo la mlima.

Matangazo

  • TANGAZO LA UKUSANYAJI NA UZOAJI TAKA HAI MJINI September 27, 2023
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA (PSLE) 2023 WILAYA YA HAI November 23, 2023
  • MAJINA YA WALIOITWA USAHILI NAFASI ZA JESHI WILAYA YA HAI September 06, 2023
  • TANGAZO LA UKUSANYAJI NA UZOAJI TAKA HAI MJINI September 27, 2023
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • Mhe Kaijage Awataka Watumishi Kufanya Kazi Kwa Bidii

    November 22, 2023
  • Mkalipa Ataka Viongozi Wa Dini Kufundisha Waumini

    November 08, 2023
  • Wananchi wa Kijiji cha Sanya Station Washukuru Ulipwaji Wa Fidia

    October 25, 2023
  • Mkurugenzi Dionis Myinga Aishukuru Kambele Kwa Msaada Wa Sementi

    October 23, 2023
  • Ona Yote

Video

UGAWAJI WA PIKIPIKI WILAYA YA HAI
Vidio Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Planrep
  • TANEPS
  • Mfumo wa Ajira za Afya
  • Blog ya Wilaya
  • Fomu ya Maombi ya Likizo
  • Fomu ya OPRAS - Walimu
  • Fomu ya OPRAS - Watumishi
  • Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba Shule za Wilaya ya Hai Mwaka 2020
  • Muundo wa Halmashauri

Viunganishi Vinavyohusiana

  • BARUA PEPE YA MALALAMIKO
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya serikali
  • TAMISEMI
  • Mfumo wa Bajeti

Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitongoji cha Bomani

    Anuani ya Posta: 27 Hai

    Simu: 0272758441

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ded@haidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai