Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya Chekimaji na Kituo cha Afya Longoi katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameagizwa kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Irando, aliwataka wakandarasi hao, Augustino Mollel, Lukio Mshana, Simon Mollel na Simon Ekarua, kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili kuruhusu wananchi kupata huduma za afya, kama ambavyo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kusogeza huduma hizo kwa wananchi, baada kutoa fedha nyingi.
Amezungumza hayo alipotembelea na kukagua mradi wa ukamilishaji wa Kituo cha Afya Chekimaji na miradi ya upanuzi wa Kituo cha Afya Longoi.
“Niwatake sasa wakandarasi, hasa vituo vya afya hivi nilivyovitembelea, tunataka wafanye kazi kwa muda unaotakiwa.Waongeze mafundi na wasicheze na muda,waongeze saa za kufanya kazi ili kukamilisha miradi hii,”amesisitiza Irando
Kuhusu madai ya wakandarasi ya kupanda kwa vifaa vya ujenzi kwamba ndiko kulikowachelewesha kukamilisha miradi, Mkuu huyo wa Wilaya alisema:
“Kumekuwa na tatizo la mfumuko wa bei za vifaa vya ujenzi, lakini hili linatokana na wao wenyewe kukaa muda mrefu bila kumaliza kazi kwa wakati. Wakandarasi wanapofanya kazi kwa wakati, bei inakuwa sio ya kuumiza na kazi inamalizika, ndiyo maana nasisitiza tufanye kazi kwa muda uliopo katika mkataba ili kuepuka kupaa kwa bei ya vifaa vya ujenzi.”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai