Katibu Tawala wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Upendo Wella amewataka wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali kuhudhuria kwenye maonesho ya Wakulima na wafugaji maarufu kama Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Njiro Mkoani Arusha ili kujifunza njia mbalimbali za kisasa katika Kilimo na ufugaji.
Wella ametoa wito huo wakati alipotembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo Mkoani Arusha kwa lengo la kujionea bidhaa mbalimbali na namna wataalamu katika sekta hizo wanavyofanya kazi ya kuelimisha.
Amesema kupitia maonesho hayo wananchi wataweza kujifunza na njia za kisasa kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji huku akiwakumbusha kuwa maonesho hayo yanatoa pia fursa ya kujifunza kuhusu sekta nyingine tofauti na Kilimo.
Hata hivyo ameeleza kuridhishwa na kuvutiwa na namna ambavyo wataalamu katika banda la Halmashauri ya wilaya ya Hai walivyojipanga na kuandaa banda ambalo limekuwa darasa bora kwa wahudhuriaji wa maonesho tangu yalipofunguliwa mwaka huu.
Aidhaa ameipongeza SIDO kwa namna walivyofanya ubunifu wa kuwafunza Vijana katika maonesho hayo.
Maonesho ya NaneNane 2020 yameanza rasmi Tarehe 01 August mwaka huu yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Kwa maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Chagua viongozi Bora 2020".
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai